Lugha Nyingine
Mafanikio Kumi ya uchumi wa China katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2023
Tarehe 24 Julai, Rais wa China Xi Jinping alipotoa mpango wa pande zote juu ya hali ya uchumi ya hivi sasa ya China na kazi husika alisema, "Baada ya mpito tulivu wa kudhibiti na kukinga maambukizi ya UVIKO-19, urejeshaji wa ukuaji wa uchumi ni mchakato wenye maendeleo yalliyo kama mawimbi yanavyoenda. Uchumi wa China una nguvu ya uhimilivu na uwezo mkubwa wa maendeleo, na msingi wake wa kuongezeka kwa muda mrefu haujabadilika." Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, China imeshuhudia ongezeko la Pato la Taifa (GDP) la asilimia 5.5, likiwa ni la kasi zaidi kuliko nchi nyingine duniani, na uchumi wa China umeonesha mafanikio kumi muhimu kama yafuatayo.
Watu wakitembelea Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Magari ya Guangzhou katika Eneo la Uagizaji na Uuzaji Nje wa Bidhaa la China huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Desemba 30, 2022. (Xinhua/Lu Hanxin)
Kwanza: "Bidhaa tatu mpya" za biashara za nje ikiwemo magari yanayotumia umeme zapata maendeleo ya kuvutia watu macho
Uuzaji wa nchi za nje wa "bidhaa tatu mpya" za biashara za nje, yaani magari yanayotumia umeme, betri za lithiamu-ioni na betri za nishati ya jua, kwa jumla umeongezeka kwa asilimia 61.6. Zaidi ya nusu ya magari yanayotumia nishati mbadala duniani yanatumika nchini China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma