Lugha Nyingine
Mtindo wa kipekee wa ujenzi wa Qilou Katika Mji wa Haikou Kusini mwa China umekuwa kivutio kikuu kwa watalii
Haikou inajivunia eneo kubwa zaidi na lililohifadhiwa vizuri zaidi la majengo ya Qilou nchini China, ambalo lilijumuishwa na Serikali ya China kwenye orodha ya kwanza ya mitaa ya kihistoria Mwaka 2009.
Majengo mengi ya Qilou katika mji huo yalijengwa mapema miaka ya 1900 na Wachina waliorudi kutoka ng'ambo wakiwa na mawazo yaliyochukuliwa kutoka kwenye usanifu wa Asia ya Kusini-Mashariki ambako walikuwa wakiishi.
Eneo hili lenye mtindo wa kipekee wa majengo limegeuka kuwa kivutio kikuu kwa watalii huko Haikou.
Picha hii iliyopigwa Agosti 26, 2023 ikionyesha mandhari ya mtaa wa kale wa majengo ya Qilou huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. Qilou, au nyumba zenye matao, inarejelea jengo lenye matao ya mbele kwenye ghorofa ya chini ambayo yanaruhusu watembea kwa miguu kupita. (Xinhua/Yang Guanyu)
Picha hii iliyopigwa Agosti 20, 2023 ikionyesha sehemu ya majengo kwenye mtaa wa kale wa Qilou huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Xinhua/Yang Guanyu)
Watalii wakionekana katika picha kwenye mtaa wa kale wa Qilou huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Agosti 21, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)
Watalii wakitembelea mtaa wa kale wa Qilou huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Agosti 21, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)
Picha hii iliyopigwa Agosti 21, 2023 ikionyesha sehemu ya majengo kwenye mtaa wa kale wa Qilou huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Xinhua/Yang Guanyu)
Watalii wakitazama onyesho kwenye mtaa wa kale wa Qilou huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Agosti 20, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)
Picha hii iliyopigwa Agosti 26, 2023 ikionyesha maelezo fulani kwenye majengo katika mtaa wa kale wa Qilou huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Xinhua/Yang Guanyu)
Sanamu zikionekana katika picha kwenye mtaa wa kale wa Qilou huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Agosti 20, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma