Tarehe 30, Agosti, mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari vya“Ukanda Mmoja, Njia Moja”la 2024 ulifanyika huko Chengdu, Li Shulei, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati kuu ya Chama, alihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano na kutoa hotuba. Washiriki wa mkutano walisema kuwa pendekezo la kujenga pamoja“Ukanda Mmoja, Njia Moja”lilitolewa na China,na matunda na fursa ni kwa dunia.
Kuanzia kutazama katuni zinazoonyesha wanyama pori utotoni hadi kuwa mhifadhi wa Wanyama pori, Zhuo Qiang, aliyepewa jina la utani Simba, ni Mchina wa kwanza anayefanya kazi ya uhifadhi wa wanyama pori barani Afrika. Mwaka 2011, Zhuo Qiang alikwenda mbuga ya Maasai Mara-Serengeti, ambapo alikuwa akiishi na Wamaasai na kufanya kazi na wahifadhi wenyeji katika Hifadhi ya Wanyama Pori ya Ol Kinyei.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian tarehe 28 alisema kuwa, kuunga mkono maendeleo ya Afrika ni jukumu la pamoja la jumuiya ya kimataifa. China inakaribisha nchi nyingine kutilia maanani kuongeza uwekezaji wao kwa Afrika kama inavyofanya China, na China ingependa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kuhimiza kwa pamoja maendeleo na ustawi wa Afrika na kuleta manufaa kwa watu wa Afrika.
Picha iliyopigwa Septemba, 2023 ikionesha stesheni ya Nairobi yareli ya Mombasa-Nairobi. (Picha na Xinhua) Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian tarehe 27 alisema, mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) 2024 utafunguliwa hivi karibuni, na upande wa China ungependa kushirikiana na upande wa Afrika katika kuendelea kung’arisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika ujenzi wa kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.