Lugha Nyingine
Wizara ya Mambo ya Nje ya China: Kung’arisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika ujenzi wa kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
Picha iliyopigwa Septemba, 2023 ikionesha stesheni ya Nairobi yareli ya Mombasa-Nairobi. (Picha na Xinhua)
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian tarehe 27 alisema, mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) 2024 utafunguliwa hivi karibuni, na upande wa China ungependa kushirikiana na upande wa Afrika katika kuendelea kung’arisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika ujenzi wa kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku hiyo, mwandishi wa habari aliuliza kuwa, hivi karibuni kuna msomi wa Afrika ambaye alisema ushirikiano wa ujenzi wa kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umefanya kazi muhimu kwa kuhimiza mafungamano ya mawasiliano kati ya nchi za Afrika, hivi sasa bara hilo bado lina pengo kubwa katika ujenzi wa miundombinu, na ushirikiano huo wa Afrika na China utahimiza maendeleo endelevu, ongezeko la uchumi na mtandao wa uchumi wa bara hilo, je, Msemaji una maoni gani kuhusu maneno hayo? Na ushirikiano wa ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” utaleta nini kwa kuhimiza mafungamano ya mawasiliano ya nchi za Afrika?
Lin alisema, ujenzi wa miundombinu ni msingi muhimu wa maendeleo ya Afrika, na kutimiza mafungmaano ya mawasiliano ni matarajio ya pamoja ya nchi za Afrika . Katika miaka mingi iliyopita, chini ya mfumo wa FOCAC na ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, China siku zote inashikilia wazo la ukweli, uhalisia, urafiki na udhati na mtazamo sahihi wa haki na faida , na kuunga mkono kithabiti nchi za Afrika kuboresha miundombinu na kuinua kiwango cha mafungamano ya mawasiliano , na kutimiza maendeleo endelevu.
"Tukitaka kuwa tajiri, bora kujenga kwanza barabara,” alisema, akiongeza kuwa kwa miaka mingi China na Afrika zimejenga na kuboresha barabara zenye urefu karibu kilomita 100,000, njia za reli zimezidi urefu wa kilomita 10,000, madaraja karibu 1,000, na bandari mia moja hivi.
“Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika 2024 utafunguliwa hivi karibuni, na ujenzi wa kiwango cha juu wa ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ utakuwa moja kati ya mada muhimu za mkutano huo.” Lin alisema, upande wa China ungependa kufanya juhudi pamoja na upande wa Afrika kwenye njia ya kusonga mbele ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, kufanya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” liendane na Ajenda ya Mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika na mikakati ya nchi za Afrika, kuendelea kung’arisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika ujenzi wa kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kusukuma ushirikiano wa mafungamano ya mawasiliano uingie kwenye njia ya maendeleo ya kasi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma