Rais wa Kenya William Ruto amesema Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka huu utaonyesha mwelekeo wa ushirikiano kati ya Afrika na China katika zama mpya, kuhimiza ukuaji wa uchumi wa kijani, kuhimiza maendeleo ya amani, na kuimarisha kufunzana kati ya ustaarabu. Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Rais Ruto amesema, Kenya inaamini kwamba Baraza hilo litaongeza msukumo mpya katika ushirikiano wa Kenya na China na kusaidia Kenya na nchi nyingi za Afrika kuelekea ujenzi wa mambo ya kisasa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi jana Jumapili hapa Beijing amekutana kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Bw.
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ameanza kufanya shughuli za pande mbili leo siku ya Jumatatu na viongozi wa kigeni ambao watahudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), unaotarajiwa kufanyika Septemba 4 hadi 6 mjini Beijing. Leo siku ya Jumatatu asubuhi Rais Xi amekutana na rais Felix Tshisekedi, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), rais Assimi Goita wa Mali, rais Faure Gnassingbe wa Togo, na rais Azali Assoumani wa Visiwa vya Comoro kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
BEIJING - Viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika wanafululiza kuwasili Beijing, Mji Mkuu wa China kwa kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika kuanzia Septemba 4-6.