BEIJING - Rais Xi Jinping wa China na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na ziara ya kiserikali siku ya Jumatatu wametangaza kupandisha hadhi ya uhusiano kati ya pande mbili kuwa ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kwa pande zote katika zama mpya. Rais Xi amesema kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini kunaendana na matarajio ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili na mchakato wa kihistoria wa maendeleo ya Nchi za Kusini.
Mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambao utafanyika Septemba 4 - 6 umefanyika mjini Beijing siku ya Jumatatu, Septemba 2.
Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) umepangwa kufanyika Beijing, China kuanzia kesho Jumatano Septemba 4 hadi siku ya Ijumaa Septemba 6 ambapo viongozi wakuu mbalimbali kutoka nchi za China na Afrika watahudhuria.
Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika kuanzia kesho Jumatano mjini Beijing na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki Dkt. Caroline Asiimwe amesema kuwa, mabadiliano na ushirikiano wa nyanja ya lugha kati ya China na Afrika yanasaidia kuunganisha mawasiliano ya watu kati ya pande hizo mbili.