Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Hussein Ali Mwinyi Jumatatu aliishukuru timu ya madaktari wa China kwa mchango wao katika kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa kichocho visiwani Zanzibar. Akizungumza na wataalamu hao wa afya kutoka China katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika Ikulu Zanzibar baada ya kumalizika kwa mradi wa kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kichocho unaofadhiliwa na China kisiwani Zanzibar, Dkt Mwinyi alisema mradi huo umesaidia makundi yaliyo katika mazingira hatarishi katika visiwa hivyo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian Jumatatu alisema China siku zote inaunga mkono Afrika katika kutafuta njia mpya ya kisasa, na pia inatoa mchango muhimu katika njia mpya ya kupunguza umaskini barani Afrika.
Gatera, Mnyarwanda mwenye umri wa miaka 31, ni mwanafunzi wa PhD katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Anhui, na kozi yake ni kuotesha mbegu za mahindi. Mwaka 2019, Gatera alikuja Hefei, Mkoa wa Anhui kusoma shahada ya uzamili kwa ufadhili wa serikali ya China na kuendelea masomo yake ya shahada ya uzamivu katika chuo kikuu hicho.
Shughuli ya kuwaaga wanafunzi wa Kenya waliopata udhamini wa masomo kutoka kwa serikali ya China kwa ajili ya kuendelea na masomo ya juu katika vyuo vikuu nchini China, imefanyika kwenye ubalozi wa China nchini Kenya. Shughuli ya kuwaaga wanafunzi 13 walionufaika na udhamini huo, iliambatana na hafla ya kuwapatia tuzo washindi wa Shindano la Insha la "China-Africa Cooperation in My Eyes".