Lugha Nyingine
China yatoa mchango muhimu katika njia mpya ya kupunguza umaskini barani Afrika
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian Jumatatu alisema China siku zote inaunga mkono Afrika katika kutafuta njia mpya ya kisasa, na pia inatoa mchango muhimu katika njia mpya ya kupunguza umaskini barani Afrika.
Lin alisema hayo alipojibu swali juu ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika kupunguza umaskini kwenye mkutano na wanahabari . Akibainisha kuwa kuondoa umaskini ni majukumu ya binadamu wote, pia ni matumaini ya watu wote wa Afrika. Lin alisema upunguzaji wa umaskini ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya China na Afrika siku zote.
Aliongeza kuwa kwa miaka mingi, China na Afrika zinatekeleza kivitendo Programu ya Kuimarisha Ushirikiano kati ya China na Umoja wa Afrika juu ya Upunguzaji wa Umaskini chini ya kanuni za udhati, matokeo halisi, upendo na nia njema na kutafuta zaidi maslahi ya pamoja. Pande mbili pia zinafanya mawasiliano na ushirikiano chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na kupata matokeo ya kidhahiri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma