Naibu rais wa Afrika Kusini Bw. Paul Mashatile amesema serikali mpya ya Afrika Kusini itaendelea kufuata kithabiti sera za kirafiki kwa China na inapenda kupanua ushirikiano na China, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo makubwa zaidi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying leo ametangaza kuwa Rais Xi Jinping wa China atahudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC wa mwaka 2024 tarehe 5, Septemba. Katika wakati wa Mkutano huo wa kilele, Rais Xi pia atafanya tafrija ya kuwakaribisha viongozi wa nchi za Afrika, mashirika ya kikanda na kimataifa walioalikwa kuhudhuria Mkutano huo na kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za pande mbili mbili.
Meli ya hospitali ya kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), “Peace Ark”, iliyo katika “Jukumu la Masikilizano 2024” imewasili katika Afrika Kusini Tarehe 22, Agosti na kuanza ziara yake kwa siku saba na kutoa huduma za matibabu. Hii ni mara ya kwanza kwa Meli ya hospitali “Peace Ark” kufanya ziara nchini Afrika Kusini.
Kenya na China jana zimesaini makubaliano kuhimiza ushirikiano wa nishati mbadala katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Kaimu ofisa mkuu mtendaji katika Shirikisho la Nishati Mbadala la Kenya Bi.