Tarehe 5, Agosti, huko Yiwu mkoani Zhejiang, China, mfanyabiashara wa Senegal Bw. Sulahat akionesha magari ya kutumia nishati mpya, magari ambayo yaliundwa na China na ameyaagiza.
Habari kutoka Maputo: Mradi wa Kituo cha usambazaji wa maji na mtandao wa mabomba ya maji uliojengwa na kampuni ya Power China huko Pemba, mji mkuu wa jimbo la Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji, ulizinduliwa rasmi tarehe 19, na Rais Nyusi wa Msumbiji alishiriki kwenye halfa na kubonyeza tufe la pampu ya maji. Rais Nyusi alisema kwenye hotuba yake kwamba kukamilika kwa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha usambazaji wa maji na mtandao wa mabomba ya maji wa Mji wa Pemba ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya ukanda wa kaskazini wa Msumbiji.