Lugha Nyingine
Mradi wa utoaji maji wa manispaa unaojengwa na kampuni ya China huko kaskazini mwa Msumbiji wazinduliwa rasmi
Habari kutoka Maputo: Mradi wa Kituo cha usambazaji wa maji na mtandao wa mabomba ya maji uliojengwa na kampuni ya Power China huko Pemba, mji mkuu wa jimbo la Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji, ulizinduliwa rasmi tarehe 19, na Rais Nyusi wa Msumbiji alishiriki kwenye halfa na kubonyeza tufe la pampu ya maji.
Rais Nyusi alisema kwenye hotuba yake kwamba kukamilika kwa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha usambazaji wa maji na mtandao wa mabomba ya maji wa Mji wa Pemba ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya ukanda wa kaskazini wa Msumbiji. Katika miaka ya hivi karibuni iliyopita, idadi ya watu wa Msumbiji imekuwa ikiendelea kuongezeka, serikali itaendelea kufanya juhudi katika ujenzi wa miundombinu na kuhimiza ujenzi na ukarabati wa mabwawa na maboma mengi na mifumo ya usambazaji wa maji ili kuendana na maendeleo ya miji na kukidhi mahitaji ya maisha ya watu.
Baada ya kuzinduliwa kwa mradi huo, ufanisi wa utoaji maji wa Mji wa Pemba utaongezeka kwa kiasi kikubwa na kuleta nguvu mpya kwa maendeleo ya huko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma