Lugha Nyingine
“Bidhaa za China” Zanunuliwa Vizuri Afrika
Tarehe 5, Agosti, huko Yiwu mkoani Zhejiang, China, mfanyabiashara wa Senegal Bw. Sulahat akionesha magari ya kutumia nishati mpya, magari ambayo yaliundwa na China na ameyaagiza.
“Angalia, hayo magari 100 ya kutumia nishati mpya ndiyo niliyoagiza kutoka China, magari ya aina hiyo yanakaribishwa sana huko Dakar!” Mfanyabiashara wa Senegal, Bw.Sulahat aliwaonesha video moja kwenye simu yake kwa waandishi wa habari.
Bw.Sulahat amesema, “nimeanzisha kampuni moja huko Dakar ambayo ni ya kutoa huduma ya kuita mtandaoni gari la kutumia nishati mpya, natarajia kuendesha kampuni yangu hiyo kwa mfano wa uendeshaji wa ‘texi za Didi’ nchini China. Amesema kuwa, kwa Senegal, kuingiza magari ya kutumia nishati mpya kutaleta manufaa mengi, si kama tu kutatoa nafasi za ajira, na kupunguza gharama za uendeshaji wa texi, bali pia kutasaidia zaidi kulinda mazingira.
Huu ni moja ya “miamko ya biashara” aliopata Sulahat. Katika Mji wa Yiwu ambao umejulikana kuwa “supamaketi ya Dunia”, Sulahat ameshuhudia mawasiliano kati ya China na Afrika yanayoongezeka siku hadi siku katika sekta za uchumi na biashara.
Kwenye ukumbi wa maonesho ya kampuni ya biashara aliyoanzisha Sulahat huko Yiwu, zimeoneshwa mifano ya bidhaa za paneli za nishati ya jua, pamoja na mamia na maelfu ya aina za vitu vya matumizi ya lazima na vyombo vya umme nyumbani. Wafanyabiashara wengi kutoka nchi za Afrika wanakuja kutembelea na kuagiza bidhaa bila kusita.
Sulahat amesema, “Hapo awali, kila mwaka nilikuwa kusafirisha makotena 20 hadi 30 ya bidhaa kutoka hapa kwa nchi za Afrika. Mwaka jana nilisafirisha makontena zaidi ya 4000 ya bidhaa za aina 1000 na zaidi kwa nchi za Afrika. Nakadiria takwimu hizo zitaongezeka mwaka huu.”
Bidhaa za China za aina nyingi mbalimbali zinanunuliwa vizuri katika nchi za Afrika siku hadi siku. Takwimu zilizotolewa zimeonesha kuwa, China imedumisha nafasi yake ya mwenzi mkubwa wa kwanza wa biashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo. Mwaka 2023, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 282.1 kwenye historia yake, ambapo magari ya kutumia nishati mpya, Betri za Lithium, na bidhaa za photovoltaic zilizouzwa barani Afrika ziliongezeka kwa 291%、109%、57% kuliko mwaka 2022.
Mfanyabiashara kutoka nchi ya Mali anachagua na kununua vipuri vya bidhaa za photovoltaic katika duka moja kwenye mtaa wa bidhaa ndogo ndogo za China huko Yiwu. (Xinhua/Weng Xinyang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma