Lugha Nyingine
Baraza la Ushirikiano wa?Vyombo vya Habari vya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”?la 2024 lafanyika Chengdu
Tarehe 30, Agosti, mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari vya“Ukanda Mmoja, Njia Moja”la 2024 ulifanyika huko Chengdu, Li Shulei, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati kuu ya Chama, alihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano na kutoa hotuba.
Washiriki wa mkutano walisema kuwa pendekezo la kujenga pamoja“Ukanda Mmoja, Njia Moja”lilitolewa na China,na matunda na fursa ni kwa dunia. Tangu mwaka 2013 Rais Xi Jinping wa China alipotoa pendekezo hilo muhimu, ushirikiano wa kimataifa wa“Ukanda Mmoja, Njia Moja”umekua kwa ustawi, na kupata matokeo halisi makubwa, ambao umechora picha nzuri ya mafungamano ya dunia na kunufaika pamoja na mafanikio.
Washiriki wa mkutano waliamini kuwa vyombo vya habari ni dirisha la kuonyesha matokeo ya maendeleo na ni kiunganishi cha kuhimiza ushirikiano wa kufuata hali halisi, wanapaswa kusimulia hadithi za ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, kubeba jukumu la kuhimiza maendeleo halisi, na kuripoti ipasavyo uzoefu wa kujenga kwa pamoja pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutoa mchango wa kuhimiza hamasa kwa ajili ya dunia.
Mkutano wa Baraza hilo uliandaliwa kwa pamoja na Gazeti la People's Daily, Kamati ya Chama ya Mkoa wa Sichuan, na Serikali ya Umma ya Mkoa wa Sichuan, na kaulimbiu yake ni "Kuendeleza kwa kina Ushirikiano wa Vyombo vya Habari na Kuhimiza Maendeleo kwa Pamoja." Wakuu, wahariri na waandishi wa habari zaidi ya 200 kutoka vyombo 191 vya habari katika nchi 76, wakuu wa idara husika, wataalamu, wasomi na wajumbe wa mashirika walihudhuria mkutano huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma