Rais Andry Nirina Rajoelina wa Madagascar akitoa hotuba kwenye Majadiliano ya Wazi ya Maendeleo ya Kiuchumi kati ya China na Madagascar 2024. (Picha na Weng Qiyu/People's Daily Online) Majadiliano ya Wazi ya Maendeleo ya Kiuchumi kati ya China na Madagascar 2024 yamefanyika hapa Beijing siku ya Alhamisi usiku, tarehe 5, Septemba ambapo Rais Andry Nirina Rajoelina wa Madagascar alishiriki kwenye shughuli hiyo na kutoa hotuba kuu, na naibu mhariri mkuu wa People’s Daily Xu Lijing alihudhuria na kutoa hotuba.
BEIJING - Peng Liyuan, mke wa Rais wa China Xi Jinping, amehudhuria mkutano kuhusu elimu ya wanawake wa China na Afrika siku ya Alhamisi na kutoa hotuba, ambapo wake wa viongozi wa Afrika wapatao zaidi ya 20, ambao wako Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), wameshiriki kwa pamoja katika shughuli za mkutano huo. Katika hotuba yake, Peng amesema China na Afrika ni za jumuiya yenye mustakabali wa pamoja na kwamba wanawake wa China na Afrika kwa bidii, hekima na kujitolea, wameandika ukurasa usio na kifani wa mshikamano, ushirikiano na maendeleo.
Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu amani na usalama wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ukifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Shen Hong) BEIJING - Viongozi wa China na Afrika wametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano katika kudumisha amani na usalama kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ulioendeshwa kwa pamoja na Cai Qi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso.
Mkutano kuhusu ushirikiano wa sifa bora wa Ukanda Mmoja, Njia Moja wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ukifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Li Xiang) BEIJING - China na nchi za Afrika zitaimarisha ushirikiano wao wenye sifa bora chini ya Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, wamesema wajumbe wa mkutano wa ngazi ya juu wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaoendelea.