Lugha Nyingine
Viongozi wa China na Afrika watoa wito wa kuimarishwa ushirikiano katika masuala ya amani na usalama
Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu amani na usalama wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ukifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Shen Hong)
BEIJING - Viongozi wa China na Afrika wametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano katika kudumisha amani na usalama kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ulioendeshwa kwa pamoja na Cai Qi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso.
Cai amesema juhudi za pamoja za China na Afrika za kujenga mambo ya kisasa juu ya msingi wa amani na usalama zitatoa mchango mkubwa zaidi kwa amani na maendeleo ya dunia.
China itahimiza kwa nguvu kubwa ushirikiano wa amani na usalama ndani ya mfumokazi wa FOCAC, kuanzisha ushirikiano na nchi za Afrika ili kutekeleza Pendekezo la Usalama wa Dunia, na kujenga maeneo ya kielelezo ya ushirikiano chini ya pendekezo hilo, Cai amesema.
Amesema China inapenda kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza amani na usalama barani Afrika.
Viongozi wa Afrika waliozungumza kwenye mkutano huo wameeleza matarajio yao kwa Afrika na China kufanya kazi pamoja katika kujenga mambo ya kisasa juu ya msingi wa amani na usalama, ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika kudumisha utulivu wa kimataifa.
Wawakilishi takriban 300 wa China na nchi za nje walihudhuria mkutano huo. Wanajumuisha wajumbe kutoka nchi zaidi ya 50 za Afrika na mashirika makubwa ya kikanda.?
Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu amani na usalama wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ukifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)
Cai Qi, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu amani na usalama wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)
Denis Sassou Nguesso, Rais wa Jamhuri ya Kongo, akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu amani na usalama wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma