Baadhi ya wanafunzi wa Kenya wanaosoma Chuo Kikuu cha Jiaotong cha Beijing, China ambao hapo awali walimwandikia barua Rais Xi Jinping wa China na kupokea jibu lake wameeleza kuwa reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi iliyojengwa na Shirika la Madaraja la China imeleta mageuzi makubwa katika sekta za uchumi na usafirishaji nchini Kenya. Wanafunzi hao walimwandikia barua Rais Xi mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kumaliza masomo yao katika chuo hicho, wakieleza shukrani zao kwake kwa kuja na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja ambalo limeleta manufaa makubwa kwa watu na nchi mbalimbali duniani ikiwemo Kenya ambayo imenufaika na miradi ya ushirikiano wa pande mbili ikiwemo miundombinu hususan reli hiyo ya SGR ya Nairobi-Mombasa ambako wanafanya kazi na fursa za ufadhili wa masomo ambazo wao ni moja ya wanufaika.
Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unafanyika kuanzia Septemba 4 hadi 6 mjini Beijing. Moja ya kumbi za mkutano huo, Kituo cha Kitaifa cha Mikutano cha China kinatoa Eneo la Uonyeshaji wa Mwingiliano wa Teknolojia na Utamaduni, likiwapa waandishi wa habari, wote wa China na wale wa kigeni, teknolojia changamani na kujionea urithi wa kitamaduni usioshikika.
Rais Xi Jinping leo tarehe 5 amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Beijing, ambapo alitangaza kuinua uhusiano kati ya China na nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kibalozi kwenye ngazi ya kimkakati, na uhusiano kati ya China na Afrika kwa ujumla ufikie kwenye jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote katika zama mpya. Rais Xi amesema katika miaka 24 iliyopita tangu kuanzishwa kwa FOCAC mwaka 2000, China na nchi za Afrika zimeelewana na kuungana mkono, na kutoa mfano wa kuigwa kwa uhusiano wa kimataifa wa aina mpya.
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amepongeza "mfano bora" wa uhusiano kati ya China na Afrika wakati China ikitandaza zulia jekundu kwa viongozi wa Afrika na wageni wengine walioko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), hii ni shughuli kubwa zaidi ya kidiplomasia inayoandaliwa na China katika miaka mingi iliyopita, ambapo Xi na mkewe, Peng Liyuan, wamefanya dhifa ya kukaribisha wageni hao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi zaidi ya 50 wa Afrika na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, umeanza rasmi jana Jumatano Septemba 4 na utaendelea hadi kesho Ijumaa Septemba 6.