Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 4 2024. (Xinhua/Li Tao) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan siku ya Jumatano, ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo amesema mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania.
(Xinhua/Zhai Jianlan) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema leo asubuhi kwa pamoja wameshuhudia hafla ya utiaji saini makubaliano ya maelewano (MoU) kuhusu mradi wa kustawisha njia ya reli ya TAZARA. Marais Samia na Hichilema wako Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
(Picha na Yin Bogu/Xinhua) Rais Xi Jinping wa China tarehe 2 alikutana na rais Faure Gnassingbe wa Togo hapa Beijing.
(Picha na Yin Bogu/Xinhua) Rais Xi Jinping wa China alikutana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi Jumatatu hapa Beijing. Tshisekedi yupo Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).