Lugha Nyingine
Peng Liyuan pamoja na wake wa viongozi wa Afrika wahudhuria mkutano kuhusu elimu ya wanawake
BEIJING - Peng Liyuan, mke wa Rais wa China Xi Jinping, amehudhuria mkutano kuhusu elimu ya wanawake wa China na Afrika siku ya Alhamisi na kutoa hotuba, ambapo wake wa viongozi wa Afrika wapatao zaidi ya 20, ambao wako Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), wameshiriki kwa pamoja katika shughuli za mkutano huo.
Katika hotuba yake, Peng amesema China na Afrika ni za jumuiya yenye mustakabali wa pamoja na kwamba wanawake wa China na Afrika kwa bidii, hekima na kujitolea, wameandika ukurasa usio na kifani wa mshikamano, ushirikiano na maendeleo.
Katika kuendeleza elimu ya wanawake na kuelekea katika mustakabali mzuri zaidi, China na Afrika zinaendana katika malengo yao, Peng ameeleza.
Kwenye mkutano huo, Marie Khone Faye, mke wa Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, na washiriki wengine wa mkutano pia walitoa hotuba.
Wamemshukuru Peng kwa mchango wake bora katika kuhimiza elimu ya watoto wa kike na wanawake wa Afrika na kusifu uungaji mkono na msaada wa muda mrefu wa China katika nyanja husika.
Peng na wageni wa Afrika pia walifurahia uimbaji wa watoto na Opera ya Beijing na vitu vya maonyesho vinavyoonyesha utamaduni wa jadi wa China na mafanikio katika elimu ya wanawake.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma