Lugha Nyingine
Majadiliano ya Wazi ya Maendeleo ya Kiuchumi kati ya China na Madagascar 2024 yafanyika Beijing
Rais Andry Nirina Rajoelina wa Madagascar akitoa hotuba kwenye Majadiliano ya Wazi ya Maendeleo ya Kiuchumi kati ya China na Madagascar 2024. (Picha na Weng Qiyu/People's Daily Online)
Majadiliano ya Wazi ya Maendeleo ya Kiuchumi kati ya China na Madagascar 2024 yamefanyika hapa Beijing siku ya Alhamisi usiku, tarehe 5, Septemba ambapo Rais Andry Nirina Rajoelina wa Madagascar alishiriki kwenye shughuli hiyo na kutoa hotuba kuu, na naibu mhariri mkuu wa People’s Daily Xu Lijing alihudhuria na kutoa hotuba.
Kwenye hotuba yake, Rais Andry Rajoelina amesema, katika miongo iliyopita China imepata mageuzi makubwa, na uzoefu na mfano wake huo wa kuigwa umetoa hamasa kwa watu wote.
Amesema, Madagascar ipo katika kipindi cha mageuzi na inahitaji washirika wa kutegemewa na kuaminika. Ameongeza kuwa kampuni za China zenye uwezo na nia ya uwekezaji zinakaribishwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa Madagascar, na anatumai kuanzisha ushirikiano lengwa katika maeneo ya kipaumbele kiuchumi kama vile nishati, kilimo, biashara na utalii.
Kwenye shughuli hiyo, wadau wa sekta ya viwanda wa nchi hizo mbili walitia saini makubaliano kadhaa ya miradi ya ushirikiano katika nyanja za ujenzi wa eneo maalumu la kiuchumi la Madagascar, sekta ya utalii, nishati na madini, kilimo cha kisasa na nyinginezo.
Majadiliano hayo ya wazi yameandaliwa kwa pamoja na Ikulu ya Madagascar, Wizara ya Mambo ya Nje ya Madagascar, Ubalozi wa Madagascar nchini China, gazeti la mtandaoni la People's Daily, na Shirikisho la Wafanyabiashara wa China na Afrika la Mji wa Wenzhou.
Rais wa People’s Daily Online Ye Zhenzhen aliongoza majadiliano hayo.
Wadau wa sekta ya viwanda wa China na Madagascar wakitia saini makubaliano ya miradi kwenye majadiliano ya wazi. (Picha na Weng Qiyu/People’s Daily Online)
Majadiliano ya Wazi ya Maendeleo ya Kiuchumi kati ya China na Madagascar 2024 yakifanyika. (Picha na Weng Qiyu/People’s Daily Online)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma