Lugha Nyingine
Magofu ya Mji wa Kale wa Gedi nchini Kenya Yaorodheshwa kwenye Orodha ya Mali ya Urithi wa Dunia ya UNESCO (6)
Watu wakitembelea magofu ya mji wa kale wa Gedi katika Kaunti ya Kilifi, Kenya, Aprili 15, 2023.(Picha ya Kumbukumbu/Xinhua/Han Xu) |
Mkutano wa 46 wa Mali ya Urithi wa Dunia wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) uliofanyika New Delhi, India, hivi karibuni umepitisha azimio la kuyaingiza magofu ya mji wa kale wa Gedi nchini Kenya kwenye Orodha ya Mali ya Urithi wa Dunia ya UNESCO. Mji huo wa kale wa Gedi, ulioko katika eneo la pwani ya Kenya, Kaunti ya Kilifi, ni mabaki ya mji wa Waswahili. Magofu yaliyopo sasa ya mji huo wa kale wa Gedi yamezungukwa na misitu minene ya asili, yakiendelea kuwa na mabaki ya nyumba za makazi, majengo ya dini, majengo ya mji na mifumo ya maji iliyokuwa imeendelezwa zaidi wakati huo. Yanaonyesha mpangilio wa mji huu uliowahi kustawi sana zamani na kuonyesha mitindo ya usanifu majengo ya ustaarabu wa Waswahili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma