Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na rais wa Vietnam To Lam (8)
|
Agosti 19, Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) alifanya mazungumzo na Rais wa Vietnam To Lam, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) anayefanya ziara ya kiserikali nchini China katika Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing. Baada ya mazungumzo, wakuu hao wawili walishuhudia kwa pamoja kutia saini nyaraka za ushirikiano kati ya pande hizi mbili katika sekta mbalimbali, zikiwemo shule ya chama, mawasiliano na muunganisho, viwanda, mambo ya fedha, ukaguzi na karantini za forodhani, afya, vyombo vya habari, serikali za mitaa na maisha ya watu. Picha hii inaonesha Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Vietnam To Lam wakishikana mikono.
(Picha na Yue Yuewei/Xinhua) |
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)