Lugha Nyingine
Ghuba ndogo ya?Sanniang?ya?Guangxi, maskani?ya pomboo weupe wa China (6)
Picha hii iliyopigwa Januari 6, 2025, ikionyesha ndama wa pomboo mweupe wa China (kushoto) akiruka katika maji karibu na Ghuba ndogo ya Sanniang mjini Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Picha na Lyu Shuai/Xinhua) |
Ghuba ndogo ya Sanniang, iliyoko kwenye Ghuba kubwa ya Beibu katika Bahari ya Kusini ya China, inajulikana kama “maskani ya pomboo weupe wa China.”
Kwa mujibu wa takwimu za timu ambayo imekuwa ikifanya utafiti wa nyangumi na pomboo katika Ghuba kuu ya Beibu kwa muda mrefu, idadi ya pomboo weupe wa China huku Ghuba ya Sanniang ikiwa sehemu yao kuu ya kuonekana mara kwa mara ni takriban 350-450.
Wakiwa ni spishi adimu iliyo hatarini kutoweka chini ya ulinzi wa kitaifa wa daraja la kwanza nchini China, pomboo hao weupe wa China walijumuishwa katika Orodha Nyekundu ya Spishi Zinazotishiwa ya Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira ya Asili (IUCN) Mwaka 2008. Wakiwa na hisia kubwa kwa ubora wa maji ya bahari, viumbe hawa wenye akili pia huchukuliwa kama kiashiria cha afya cha mfumo wa ikolojia wanaoishi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma