Lugha Nyingine
Bustani ya Wanyama ya Locajoy ya Chongqing, China yafanya sherehe ya panda wanne
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 02, 2025
Picha hii iliyopigwa Januari 1, 2025 ikimuonyesha panda kwenye Bustani ya Wanyamapori ya Locajoy katika Eneo la Yongchuan la Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua/Wang Quanchao) |
Katika siku ya kwanza ya Mwaka Mpya wa 2025, Bustani ya Wanyama ya Locajoy katika Eneo la Yongchuan la Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China ilifanya sherehe kwa ajili ya panda wake wanne, kuadhimisha mwaka wao wa kwanza tangu kuwasili katika bustani hiyo.
Tangu kuwasili kwao katika bustani hiyo mwaka jana, panda hao wanne wamezoea kwa mafanikio mazingira yao mapya chini ya uangalizi makini wa watunzaji wao. Maisha yao tulivu na mwonekano wao wa kupendeza vimeleta furaha nyingi kwa watembeleaji wa bustani hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma