Lugha Nyingine
Picha: Mrithi wa Ngoma ya jadi ya Reba ya Xizang (5)
Ani, mwenye umri wa miaka 60, ni mrithi wa Ngoma ya Jadi ya Reba. Ngoma ya Reba ni aina moja ya ngoma, ambayo imeunganisha maonesho ya michezo ya sanaa, ikijumuisha usimulizi wa hadithi, uimbaji, dansi na sarakasi. Mwaka 2006, ngoma hiyo imewekwa kwenye orodha ya kundi la kwanza la Mali ya urithi wa utamaduni usioshikika wa China. Ani alijifunza Ngoma ya Reba kutoka kwa mama yake alipokuwa na umri wa miaka 14, na amefanya juhudi kubwa kwa miaka 46 ili kupata ujuzi kamili wa michezo hiyo ya ngoma . Katika miaka ya hivi karibuni, ametoa mafunzo kwa zaidi ya wanafunzi 100 ili kuhifadhi ngoma hii ya jadi. Anatumaini wanafunzi wake wataweza kupeleka ngoma hii kwenye majukwaa mengi zaidi, ili watazamaji wengi zaidi wataweza kuhisi mvuto na haiba yake ya kipekee.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma