Lugha Nyingine
Kazakhstan yamkaribisha Rais wa China kwa ndege zikitoa moshi mwekundu na wa njano (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2024
Rais Xi Jinping wa China akishiriki kwenye hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev mjini Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan) |
ASTANA - Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev aliandaa hafla ya kumkaribisha Rais wa China Xi Jinping ambaye yuko ziarani nchini humo, ambapo ndege sita za kivita, zikiwa zimeruka juu ya ikulu ya rais, ziliacha nyuma moshi wa rangi nyekundu na njano, ambazo ni rangi za bendera ya Taifa la China.
Rais Xi aliwasili Astana siku ya Jumanne kwa ziara ya kiserikali nchini Kazakhstan, ambako pia atahudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai.
Ndege tatu za kivita za Jeshi la Anga la Kazakhstan ziliruka angani na kuisindikiza ndege ya Rais Xi baada ya ndege hiyo kuingia kwenye anga ya nchi hiyo. Tokayev alifanya hafla kubwa ya makaribisho kwenye uwanja wa ndege.?
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma