Lugha Nyingine
Mbinu za kikemikali na kibaolojia zasaidia kurejesha vitabu vya kale katika hali ya awali kaskazini mwa China (3)
Gao Xuemiao akichagua sampuli za karatasi kwa ajili ya kurejesha kitabu cha kale katika hai ya awali kwenye Maktaba ya Tianjin ya China Aprili 22, 2024. (Xinhua/Sun Fanyue) |
TIANJIN – Katika Maktaba ya Tianjin katika Mji wa Tianjini, Kaskazini mwa China vinahifadhiwa vitabu vya kale 590,000, na maktaba hiyo imekuwa ikifanya kazi ya kurejesha vitabu hivyo vya kale katika hali ya awali kwa zaidi ya miaka 70, ambapo Gao Xuemiao mwenye umri wa miaka 38 ambaye ni mtaalam wa kwanza wa kurejesha vitabu vya kale katika hali ya awali kwa taaluma ya kemia tangu kuanzishwa kwa maktaba hiyo Mwaka 1978, anaongoza timu ya kurejesha vitabu hivyo vya kale katika hali ya awali kwenye maktaba hiyo.
Siku hizi, kazi ya kurejesha vitabu vya kale katika hali ya awali imechukuliwa zaidi kuwa mchakato wa kuhusisha taaluma mbalimbali. Kuingizwa kwa mbinu za kikemikali na kibaolojia kunaufanya mchakato huo kuwa wa njia ya kisayansi zaidi.
"Tunafanya uchanganuzi wa kikemikali kabla ya mchakato wa kurejesha vitabu vya kale katika hali ya awali, ili kupata karatasi inayooana, na kupanga mipango mahsusi kwa kila kitabu cha kale," Gao amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma