Lugha Nyingine
Sarakasi za kijadi zang'ara katika Mji wa Wuqiao, mkoani Hubei, Kaskazini mwa China (7)
Wanasarakasi wakifanya mazoezi ya kawaida katika wilaya ya Wuqiao, Cangzhou, mkoani Hebei, Kaskazini mwa China. (People's Daily Online/Zhao Zhao) |
Wilaya ya Wuqiao huko Cangzhou, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, imejumuisha ufundishaji na maonyesho ya sarakasi katika utamaduni wake tangu miaka ya 1990.
Ili kukuza aina hii ya sanaa ya kijadi, wilaya hiyo ilianzisha Shule ya Sanaa ya Sarakasi ya Wuqiao Hebei na Ulimwengu wa Sarakasi ya Wuqiao. Taasisi hizi zimezalisha na kukuza idadi kubwa ya watendaji katika uwanja huu.
Maonyesho ya sarakasi ya Wuqiao ni mfano mzuri wa uonyeshaji wa vipaji mbalimbali, vinavyojumuisha michezo 486 katika kategoria 7. Hizi zinahusisha ustadi wa mwili, ustadi wa kutumia vifaa, ustadi wa kupanda farasi n.k. Maonyesho mengi yanayofanyika hapa yamepata Tuzo ya Sarakasi ya Chrysanthemum ya Dhahabu ya China, ambayo ni kilele cha kutambuliwa nchini China kwa sarakasi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma