Lugha Nyingine
Mji wa Qingzhen wa China: Mandhari Nzuri ya Milima na Maziwa Yaonekana wazi
Mji wa Qingzhen wa Mkoa wa Guizhou, China ni kituo cha viwanda cha mkoa huo, pia ni moja kati ya wilaya 100 zinazostawi zaidi Magharibi mwa China, na ni moja ya wilaya zenye nguvu zaidi ya kiuchumi za mkoa wa Guizhou.
Katika eneo la Mji wa Qingzhen, kuna watu wa makabila 45 madogo madogo wanaoishi huko, kama vile kabila la Wamiao na kabila la Wabuyi; mito mitatu ya Yachi, Maotiao na Anliu inazunguka mji huo wa wilaya, ambapo maziwa manne ya Ziwa Hongfeng, Ziwa Baihua, Ziwa Dongfeng na Ziwa Suofeng yanaufanya mji huo kung’ara zaidi.
Katika maziwa hayo, Ziwa Hongfeng ni kivutio cha utalii cha kitaifa, ambako watalii wanapotembelea hapa wanavutiwa sana na mandhari nzuri ya milima ya kijani na maji safi, na kuvutiwa na kung'ang'ania kwenye Daraja la Huayudong lililotunukiwa na tuzo ya Gustav Lindenthal, ambayo husifiwa kuwa ni “tuzo ya Nobel kwenye sekta ya ujenzi wa daraja”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma