Lugha Nyingine
Misemo iliyonukuliwa na Rais wa China Xi Jinping (2)
Kama msemo wa Afrika usemavyo, "Mto una kina kirefu kwa sababu ya chanzo chake." Mazungumzo ya kirafiki kati ya China na Afrika yalianza muda mrefu. Katika miaka ya 1950 na 60, viongozi waanzilishi wa China Mpya - Mao Zedong, Zhou Enlai na wengine - na viongozi wa Afrika wa kizazi cha zamani walianzisha zama mpya katika uhusiano wa China na Afrika. Tangu wakati huo, watu wa China na Afrika wamekuwa wakisaidiana kwa dhati na kushirikiana kwa karibu katika harakati za kupiga vita ukoloni na ubeberu na kupata uhuru na ukombozi wa nchi, na kutafuta maendeleo na ustawishaji wa taifa. Uhusiano wa kindugu umeanzishwa katika mchakato huu ambao umeshuhudia kutupitisha dhiki na faraja.
—— Hotuba ya Rais wa China Xi Jinping katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere nchini Tanzania Machi 25, 2013
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma