Watu waomboleza vifo vilivyotokana na kukanyagana kwenye msongamano wa Halloween huko Seoul, Korea
|
Watu wakiweka maua kwenye mimbari ya maombolezo iliyowekwa Seoul Plaza huko Seoul, Korea Kusini, Novemba 1, 2022. Idadi ya waliofariki kwenye tukio la mkanyagano kwenye msongamano, lililotokea Jumamosi usiku katika Wilaya ya Itaewon, mji mkuu wa Korea Kusini wa Seoul kwenye mikusanyiko ya Halloween, imeongezeka. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya Korea Kusini hadi kufikia jana Jumanne takriban watu 156 walikuwa wamefariki dunia na wengine 151 kujeruhiwa katika tukio hilo. Serikali ya Korea Kusini imetangaza kipindi cha maombolezo ya kitaifa cha wiki moja hadi Novemba 5. (Xinhua/Wang Yiliang) |
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)