Kuanzia kutazama katuni zinazoonyesha wanyama pori utotoni hadi kuwa mhifadhi wa Wanyama pori, Zhuo Qiang, aliyepewa jina la utani Simba, ni Mchina wa kwanza anayefanya kazi ya uhifadhi wa wanyama pori barani Afrika. Mwaka 2011, Zhuo Qiang alikwenda mbuga ya Maasai Mara-Serengeti, ambapo alikuwa akiishi na Wamaasai na kufanya kazi na wahifadhi wenyeji katika Hifadhi ya Wanyama Pori ya Ol Kinyei.
Gatera, Mnyarwanda mwenye umri wa miaka 31, ni mwanafunzi wa PhD katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Anhui, na kozi yake ni kuotesha mbegu za mahindi. Mwaka 2019, Gatera alikuja Hefei, Mkoa wa Anhui kusoma shahada ya uzamili kwa ufadhili wa serikali ya China na kuendelea masomo yake ya shahada ya uzamivu katika chuo kikuu hicho.
Meli ya hospitali ya kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), “Peace Ark”, iliyo katika “Jukumu la Masikilizano 2024” imewasili katika Afrika Kusini Tarehe 22, Agosti na kuanza ziara yake kwa siku saba na kutoa huduma za matibabu. Hii ni mara ya kwanza kwa Meli ya hospitali “Peace Ark” kufanya ziara nchini Afrika Kusini.