BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amepongeza "mfano bora" wa uhusiano kati ya China na Afrika wakati China ikitandaza zulia jekundu kwa viongozi wa Afrika na wageni wengine walioko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), hii ni shughuli kubwa zaidi ya kidiplomasia inayoandaliwa na China katika miaka mingi iliyopita, ambapo Xi na mkewe, Peng Liyuan, wamefanya dhifa ya kukaribisha wageni hao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi zaidi ya 50 wa Afrika na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, umeanza rasmi jana Jumatano Septemba 4 na utaendelea hadi kesho Ijumaa Septemba 6.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 4 2024. (Xinhua/Li Tao) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan siku ya Jumatano, ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo amesema mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania.
(Xinhua/Zhai Jianlan) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema leo asubuhi kwa pamoja wameshuhudia hafla ya utiaji saini makubaliano ya maelewano (MoU) kuhusu mradi wa kustawisha njia ya reli ya TAZARA. Marais Samia na Hichilema wako Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
(Picha na Yin Bogu/Xinhua) Rais Xi Jinping wa China tarehe 2 alikutana na rais Faure Gnassingbe wa Togo hapa Beijing.