Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Kenya William Ruto, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) 2024 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Kenya William Ruto, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo ameeleza kuwa nchi hizo mbili zimekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza pamoja ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na kukamilisha miradi mingi ya miundombinu muhimu zaidi, yenye ushawishi zaidi, na ni ya alama zaidi, ikichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya kikanda na kunufaisha watu wa pande hizo mbili.
Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais Bola Tinubu wa Nigeria, ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na ziara ya kiserikali, katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen) BEIJING - Rais Xi Jinping wa China na Rais Bola Tinubu wa Nigeria ambaye yuko mjini Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na ziara ya kiserikali wamefanya mazungumzo siku ya Jumanne na kutangaza kuinua uhusiano kati ya China na Nigeria kuwa uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote.
Mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambao utafanyika Septemba 4 - 6 umefanyika mjini Beijing siku ya Jumatatu, Septemba 2.