Lugha Nyingine
Habari picha: Mrithi wa ufundi wa jadi wa kutengeneza vinyago vya uso vya Kitibet mkoani Xizang, China (3)
Shilok ni mrithi wa ufundi wa jadi wa kutengeneza vinyago vya uso vya Kitibet mkoani Xizang, China, ambavyo ni urithi wa utamaduni usioshikika wa kieneo, na kazi ya utengenezaji wa kinyago ina taratibu zinazotumia muda mwingi ikiwa ni pamoja na uchongaji, kuweka matabaka, kukausha hewani na kupaka rangi.
Mwaka 2012, Shilok alianzisha ushirika wa kutengeneza vinyago vya michezo ya Sanaa ya opera ya Tibet chini ya msaada wa serikali ya mtaa na kuanza kufanya kazi hapa na wanafunzi wake. "Oda zetu nyingi zinatoka kwa makundi ya opera ya Tibet," Shilok amesema.
Katika miaka ya hivi karibuni, ushirika huo umetoa nafasi kwa wenyeji kujifunza ujuzi wa kutengeneza vinyago, kutoa nafasi za ajira, na kuchangia katika uhifadhi na maendeleo ya urithi wa utamaduni huo usioshikika.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma