Lugha Nyingine
Picha: Maajabu ya mazingira ya asili na mwonekano wa Mji wa Shenzhen, China kutokea Mlima Wutong (4)
Mlima Wutong uko katika Mji wa Shenzhen, mkoani Guangdong, China. Una urefu wa mita 943.7 kutoka usawa wa bahari na ni mlima wenye kilele kirefu zaidi katika mji huo wa Shenzhen.
Kivutio cha Watalii cha Mlima Wutong kinavuka maeneo matatu ya Luohu, Yantian, na Longgang ya Mji wa Shenzhen, na kinaungana na safu za milima ya Xinjie na vijito vya eneo la Hong Kong.
Kwa kupanda Mlima Wutong, unaweza kutazama mji wa Shenzhen kutoka juu, na wakati huohuo unaweza kuona milima na majengo ya eneo la Xinjie la Hong Kong kwa mbali.
Kwa uzuri wake wa kipekee wa mazingira ya asili na utazamaji wa mandhari ya mji, Kivutio hicho cha Watalii cha Mlima Wutong kimekuwa mahali pazuri kwa wakazi wa Shenzhen na watalii kupanda juu na kuwa karibu na mazingira ya asili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma