Lugha Nyingine
Treni ya kwanza ya mizigo ya "Jinbo" ya China-Ulaya yawasili Shanghai, Mashariki mwa China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 21, 2024
Treni ya kwanza ya mizigo ya "Jinbo" ya China-Ulaya iliyobeba vitu vya kuoneshwa kwenye Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) imewasili kwenye Stesheni ya Reli ya Minhang mjini Shanghai, Mashariki mwa China siku ya Jumapili, ikiwa ni mwaka wa nne mfululizo kwa bidhaa za maonyesho ya CIIE kusafirishwa hadi Shanghai kupitia huduma hiyo ya treni ya mizigo ya China-Ulaya.
"Jinbo" ni ufupi wa maneno ya CIIE ya Kichina. Treni hiyo, iliyosafiri umbali wa kilomita zaidi ya 11,000 kwa siku 21, imepakia makontena 76 yenye urefu wa futi ishirini yaliyobeba bidhaa zenye thamani ya Yuan milioni 100 (dola za Kimarekani kama milioni 14.08), zikiwa pamoja na vipodozi na mashine na vifaa.?
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma