Lugha Nyingine
Shamba la Chumvi lakaribisha msimu wa mavuno ya chumvi huko Caofeidian, Mkoa wa Hebei, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 17, 2024
Sasa ni msimu wa kuvuna chumvi ya majira ya mpukutiko, na wafanyakazi katika Shamba la Chumvi la Nanbao huko Caofeidian, Mji wa Tangshan wa Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, wanatumia vizuri fursa ya hali nzuri ya hewa kuvuna chumvi.
Kwa mujibu wa ripoti husika, Shamba la Chumvi la Nanbao ni moja kati ya vituo vikubwa zaidi vya uzalishaji wa chumvi ya baharini katika Eneo la chumvi la Changlu la China, likichukua eneo lenye ukubwa wa mu 350,000 (sawa na hekta 23,333.33 hivi), na mwaka huu uzalishaji wake wa jumla unakadiriwa kuja kufikia tani milioni 1.4.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma