<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>

    久久精品蜜芽国产亚洲av,国产成人观看免费全部完,1024综综合合久久AV,午夜国产成人精品,国产精品综合承认,国产高跟黑色丝袜在线

    Walinzi wa tumbili wa dhahabu wenye pua fupi kwenye Hifadhi ya Mazingira ya Asili Kusini Magharibi mwa China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2024
    Walinzi wa tumbili wa dhahabu wenye pua fupi kwenye Hifadhi ya Mazingira ya Asili Kusini Magharibi mwa China
    Tang Yulin (kulia), Tang Xiaogang (katikati) na Liu Xin, mwanafunzi mhitimu wa baiolojia wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Magharibi mwa China, wakiondoa nyasi wakati wa doria yao kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Baihe katika Wilaya ya Jiuzhaigou, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, Oktoba 11, 2024. (Xinhua/Wang Xi)

    Tang Yulin ni mlinzi wa msitu wa Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Baihe, katika Wilaya ya Jiuzhaigou, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, ambayo ni maskani ya tumbili pori 1,700 wa dhahabu wa Sichuan wenye pua fupi, spishi ambayo iko chini ya ulinzi wa ngazi ya juu zaidi wa serikali ya China.

    Tang Guoshun, babu mkubwa wa Tang Yulin, alikuwa mmoja kati ya wafanyakazi wa kwanza wa hifadhi hiyo ya mazingira ya asili ilipoanzishwa mwaka 1963. Baadaye Tang Daihui, baba yake Tang Yulin pia alijiunga na timu hiyo. Mwaka 1990, Tang Yulin aliyekuwa na umri wa miaka 22 alianza kubeba jukumu hilo kama tu alivyofanya babu na baba yake, akifanya kazi ya kuwa mlinzi wa msitu na kulinda tumbili kwenye hifadhi hiyo.

    Kutokana na njia za milimani na ukosefu wa nishati ndani ya hifadhi hiyo, doria ya kila siku ilikuwa yenye kuchosha sana kwa Tang Yulin katika miaka ya 1990. Ili kufuatilia na kurekodi alama za nyayo na tabia za maisha ya tumbili hao wa dhahabu wa Sichuan, ilimbidi kuamka mapema na kumaliza kifungua kinywa chake kufikia saa 10 alfajiri. Katika siku hizo za zamani, Tang Yulin alitumia siku kuchwa na kucha zaidi 200 kila mwaka mlimani, akibeba chakula na kujenga makazi mwenyewe.

    Shukrani kwa miaka ya juhudi katika ulinzi wa ikolojia na ujenzi wa miundombinu, mazingira ya kufanya kazi kwa walinzi wa misitu katika hifadhi hiyo yameweza kuboreshwa, na tumbili hao wa dhahabu wa Sichuan wenye pua fupi wamezoea kuwa na uhusiano wa karibu na binadamu. Kwa sasa idadi ya tumbili wa dhahabu wa Sichuan wenye pua fupi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Baihe ni ya juu zaidi miongoni mwa hifadhi za China.

    Mwaka 2019, mpwa wa Tang Yulin, Tang Xiaogang, pia alianza kuwa mlinzi wa msitu wa hifadhi hiyo.

    “Tumbili hula majani kwenye miti, na ninakula biskuti chini ya miti. Hivyo ndivyo taratibu tumejenga kuaminiana kwetu. Ni jambo la heshima sana kwangu mimi kwamba tumbili wanaishi vizuri hapa,” amesema Tang Yulin.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha

    久久精品蜜芽国产亚洲av
    <sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
    <noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>