Lugha Nyingine
Walinzi wa tumbili wa dhahabu wenye pua fupi kwenye Hifadhi ya Mazingira ya Asili Kusini Magharibi mwa China (2)
Tang Yulin ni mlinzi wa msitu wa Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Baihe, katika Wilaya ya Jiuzhaigou, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, ambayo ni maskani ya tumbili pori 1,700 wa dhahabu wa Sichuan wenye pua fupi, spishi ambayo iko chini ya ulinzi wa ngazi ya juu zaidi wa serikali ya China.
Tang Guoshun, babu mkubwa wa Tang Yulin, alikuwa mmoja kati ya wafanyakazi wa kwanza wa hifadhi hiyo ya mazingira ya asili ilipoanzishwa mwaka 1963. Baadaye Tang Daihui, baba yake Tang Yulin pia alijiunga na timu hiyo. Mwaka 1990, Tang Yulin aliyekuwa na umri wa miaka 22 alianza kubeba jukumu hilo kama tu alivyofanya babu na baba yake, akifanya kazi ya kuwa mlinzi wa msitu na kulinda tumbili kwenye hifadhi hiyo.
Kutokana na njia za milimani na ukosefu wa nishati ndani ya hifadhi hiyo, doria ya kila siku ilikuwa yenye kuchosha sana kwa Tang Yulin katika miaka ya 1990. Ili kufuatilia na kurekodi alama za nyayo na tabia za maisha ya tumbili hao wa dhahabu wa Sichuan, ilimbidi kuamka mapema na kumaliza kifungua kinywa chake kufikia saa 10 alfajiri. Katika siku hizo za zamani, Tang Yulin alitumia siku kuchwa na kucha zaidi 200 kila mwaka mlimani, akibeba chakula na kujenga makazi mwenyewe.
Shukrani kwa miaka ya juhudi katika ulinzi wa ikolojia na ujenzi wa miundombinu, mazingira ya kufanya kazi kwa walinzi wa misitu katika hifadhi hiyo yameweza kuboreshwa, na tumbili hao wa dhahabu wa Sichuan wenye pua fupi wamezoea kuwa na uhusiano wa karibu na binadamu. Kwa sasa idadi ya tumbili wa dhahabu wa Sichuan wenye pua fupi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Baihe ni ya juu zaidi miongoni mwa hifadhi za China.
Mwaka 2019, mpwa wa Tang Yulin, Tang Xiaogang, pia alianza kuwa mlinzi wa msitu wa hifadhi hiyo.
“Tumbili hula majani kwenye miti, na ninakula biskuti chini ya miti. Hivyo ndivyo taratibu tumejenga kuaminiana kwetu. Ni jambo la heshima sana kwangu mimi kwamba tumbili wanaishi vizuri hapa,” amesema Tang Yulin.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma