Lugha Nyingine
Maonyesho ya Biashara ya 136 ya Canton yaanza, yakileta fursa pana zaidi za soko kwa washirika (7)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2024
Wanunuzi wakitembelea sehemu ya maonyesho ya vyombo vya umeme vya nyumbani kwenye Maonyesho ya 136 ya Uagizaji na Uuuzaji Nje Bidhaa ya China huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Liu Dawei) |
GUANGZHOU - Maonyesho ya 136 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China, kwa ufupi yanaitwa Maonyesho ya Biashara ya Canton, yakiwa na kaulimbiu ya “Kuhudumia maendeleo ya sifa bora, kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu," yameanza jana Jumanne huko Guangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China yakivutia wafanyabiashara zaidi ya 30,000 wanaoonyesha bidhaa mpya milioni 1.15.
Kampuni, bidhaa, teknolojia na aina nyingi mpya za biashara zinaoneshwa kwa mara ya kwanza, zikivutia wanunuzi 147,000 wa ng'ambo ambao walijiandikisha mapema kwa ajili ya maonyesho hayo.
Maonyesho hayo ya biashara yatafanyika kwa vipindi vitatu kuanzia Oktoba 15 hadi Novemba 4.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma