Lugha Nyingine
Mapato ya Mfereji wa Suez nchini Misri yapungua kwa asilimia 60 tangu mwanzo wa Mwaka 2024 (8)
Meli ikisafiri majini kwenye Ghuba ya Suez, Misri, tarehe 8 Oktoba 2024. (Xinhua/Sui Xiankai) |
CAIRO - Mapato ya Mfereji wa Suez nchini Misri yamepungua kwa asilimia 60 na idadi ya meli zinazopita kwenye njia hiyo ya maji imepungua kwa asilimia 49 tangu mwanzoni mwa Mwaka 2024, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez (SCA) Osama Rabie amesema katika taarifa iliyotolewa Jumapili akiongeza kuwa "hali ya sasa na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika eneo la Bahari Nyekundu" vimewalazimisha wasafirishaji kutafuta njia mbadala za usafiri wa mbali na Mfereji wa Suez.
Takwimu zilizotolewa na SCA zimeonesha kuwa, mapato yamepungua kutoka dola bilioni 9.4 za Kimarekani zilizopatikana katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 hadi dola bilioni 7.2 katika mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Mwaka wa fedha nchini Misri huanza Julai Mosi na kumalizika Juni 30 ya mwaka unaofuata.
Tangu kuzuka kwa mgogoro wa Gaza Oktoba mwaka jana, kundi la Houthi la Yemen limekuwa likishambulia mara kwa mara meli ambazo zina uhusiano na Israeli katika Bahari Nyekundu.
Mfereji wa Suez ni chanzo muhimu cha fedha za kigeni kwa Misri, nchi ambayo bado inakabiliana na matatizo ya kiuchumi.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma