Lugha Nyingine
Safari za abiria zaongezeka maradufu wakati likizo ya Siku ya Taifa ya China inapokamilika (6)
Abiria wakitembea kwenye kando ya njia ya reli katika Stesheni ya Reli ya Yantai, Mkoani Shandong, Mashariki mwa China, Oktoba 6, 2024. (Picha na Sun Wentan/Xinhua) |
BEIJING - Sekta ya reli ya China imeshuhudia ongezeko maradufu la msongamano wa abiria siku ya Jumatatu wakati wasafiri walipokuwa wakirejea kutoka kwenye likizo ndefu ya wiki nzima ya Siku ya Taifa ambapo mtandao wa reli ulikuwa ukikadiriwa kusafirisha abiria milioni 19.86 Jumatatu, siku ya mwisho ya likizo hiyo, Kundi la Kampuni za Reli za China limesema.
Treni jumla ya 13,103 zilikuwa zikifanya kazi siku hiyo, zikiwemo treni 1,705 za ziada zilizokuwa zimepangwa kukidhi mahitaji yanayoongezeka. Hii inaashiria kiwango cha juu katika historia kwa uwezo wa kufanya kazi kwa siku moja, kundi hilo limesema.
Katika kipindi cha siku 10 za safari za likizo, kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 8, mtandao huo wa reli wa China ulikuwa umekadiriwa kusafirisha abiria milioni 175.
Ili kukidhi ongezeko la usafiri, China ilichukua hatua za kuongeza treni za ziada kwenye njia zenye wasafiri wengi na kuimarisha huduma ili kuhakikisha usafiri salama na wenye utaratibu kwa abiria.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma