Lugha Nyingine
Ndege ya Y-20?yawasili?Afrika Kusini kwa Mara ya Kwanza na kushiriki?Maonyesho ya Anga na Ulinzi ya Afrika (3)
Ndege ya Y-20 ya Jeshi la Anga la China ikishiriki kwa mara ya kwanza kwenye Maonyesho ya Anga na Ulinzi ya Afrika huko Pretoria, mji mkuu wa Afrika Kusini, Septemba 18. (Xinhua/Wang Ruijie) |
Ndege ya Y-20 ya Jeshi la Anga la China imeshiriki kwenye Maonyesho ya Anga na Ulinzi ya Afrika yaliyofunguliwa huko Pretoria, mji mkuu wa Afrika Kusini, Septemba 18 ikiwa ni mara ya kwanza kwa ndege hiyo kuwasili Afrika Kusini na itaonyeshwa ikiwa imetua na wakati ikifanya maonyesho ya anga.
Wakati wa maonyesho hayo ya anga Ndege ya Y-20 imepangwa kukamilisha miruko mitano ya kistadi kwa dakika 10.
"Ili kuonyesha mwonekano bora kwenye maonyesho, tulibuni miruko ya kistadi angani kulingana na sifa za anga za uwanja wa ndege husika na muda uliopangwa wa onyesho, na kujitahidi kuonyesha ufanisi bora wa kuruka wa ndege ya Y-20 na pia kuonyesha mbinu bora na uwezo mzuri wa marubani wa Jeshi la Anga la China." Mkuu wa marubani anayesimamia kazi hiyo Liang Yao amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma