Lugha Nyingine
Xi Jinping akagua Mji Baoji wa Mkoa wa Shaanxi na Mji Tianshui wa Mkoa wa Gansu, China (8)
Kuanzia mchana wa tarehe 10 hadi asubuhi ya tarehe 11 mwezi huu, Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China alikagua Mji Baoji wa Mkoa wa Shaanxi na Mji Tianshui wa Mkoa wa Gansu nchini China.
Katika Mji Baoji, Xi alikagua Jumba la Makumbusho la Vyombo vya Shaba Nyeusi la Baoji na Bustani ya Ikolojia ya Mto Weihe, ambapo alifahamishwa kuhusu hali ya sehemu hiyo kuimarisha uhifadhi na matumizi ya mabaki ya kale ya utamaduni, na kulinda mazingira ya asili ya Mto Weihe.
Kwenye Mji Tianshui, Xi alikagua Hekalu la Fuxi, Mashamba ya Tufaha ya Nanshan kwenye eneo la Maiji, na Mapango ya Mawe ya Mlima Maijishan, ambapo alifahamishwa kuhusu hali ya sehemu hiyo kuhimiza kazi ya kuhifadhi na kurithisha mabaki ya kale ya utamaduni, na ya kuendeleza viwanda vya kisasa vya kuzalisha bidhaa za matunda yenye sifa ya kipekee ya sehemu ya milimani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma