Lugha Nyingine
Mashindano ya Mbio za Magari kuvuka Jangwa za Kubuqi ya China 2024?na Michuano ya Hadhara ya Magari kuvuka Jangwa ya China ya Kituo cha Hangjinqi yaanza
Tarehe 22 Agosti, Mashindano ya Mbio za Magari kuvuka Jangwa za Kubuqi ya China 2024, pia ni Michuano ya Hadhara ya Magari kuvuka Jangwa ya China ya Kituo cha Hangjin yalifunguliwa kwenye Uwanja wa Sini wa Wilaya ya Hangjin ya Mji wa Ordos, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, China.
Zhang Zhongping, naibu katibu wa Kamati ya Chama ya Wilaya ya Hangjin ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, alisema katika hafla ya ufunguzi kwamba Wilaya ya Hangjin itajitahidi kufanya mashindano hayo kuwa ya kipekee na kujenga Wilaya ya Hangjin kuwa sehemu yenye nguvu ya kufanya mashindano ya kuvuka jangwa na kuwa nyumbani kwa madereva.
Katika miaka ya hivi karibuni, wilaya ya Hangjin imetafuta kwa nguvu uwezo wa kitamaduni wa eneo hilo, imetumia vya kutosha nguvu yake bora ya rasilimali na chapa, na kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha maendeleo ya shughuli za utalii na utamaduni ili kupanua ushawishi na umaarufu wa shughuli za utalii katika wilaya hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma