Lugha Nyingine
Mkandarasi wa China apata mafanikio ya kupitika kwa handaki la mwisho kwenye njia kuu ya usafiri wa haraka Nepal (2)
KATHMANDU – Handaki la mwisho limefaulu kupasuliwa na kupitika siku ya Jumatatu kwa mradi wa pili ulio chini ya kandarasi ya kampuni ya China chini ya mradi wa ujenzi wa njia kuu ya usafiri wa haraka wa Kathmandu-Terai/Madhesh, ambapo Waziri Mkuu wa Nepal KP Sharma Oli ameuelezea kuwa ni "hatua muhimu" katika kufikia malengo ya maendeleo ya Nepal.
Baada ya waziri mkuu kubonyeza kitufe, mlipuko wa mwisho ulilipuliwa na kupasua sehemu ya mwisho ya handaki la kushoto la Dhedre.
"Kushuhudia mafanikio ya kupitika kwa handaki lingine ni jambo la furaha," Oli amesema kwenye hafla ya mafanikio hayo iliyofanyika katika mahali pa ujenzi wa mradi huo katika wilaya ya Makwanpur.
Handaki la Dhedre na handaki la Lanedanda ni sehemu ya mradi wa pili chini ya mradi wa ujenzi wa njia kuu ya usafiri wa haraka, ambao pia unahusisha ujenzi wa madaraja makubwa mawili, miongoni mwa mengine.
Mwezi Mei 2021, Kampuni ya Uhandisi ya Poly Changda ya China ilitia saini makubaliano ya kandarasi na Jeshi la Nepal kuhusu mradi huo wa 2 wa ujenzi wa njia kuu ya usafiri wa haraka, ambayo ina urefu wa kilomita 4.62.
Mahandaki yote mawili yanajumuisha handaki la kushoto na kulia, huku ujenzi wa mahandaki mawili ya Lanedanda ukiwa ulikamilishwa mwezi wa Mei na Julai, na handaki la kulia la Dhedre lilipasuliwa mwezi wa Mei.
Akihutubia hafla hiyo ya mafanikio, Balozi wa China nchini Nepal Chen Song amezungumzia kuanzishwa kwa vifaa vya teknolojia ya hali ya juu vya ujenzi wa kiotomatiki wa handaki kama vile mashine ya mikono mitatu ya kuchimba miamba na mikono ya roboti ya kunyunyizia maji kwa ajili ya mradi huo.
Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Kando Mbili za Mfereji Mkuu wa China Yaonyeshwa Mkoani Hebei
Michezo ya Kupanda Farasi ya"Agosti Mosi" yaanza katika Wilaya ya Litang Mkoa wa Sichuan, China
Mashindano ya kimataifa ya boti za matanga yamalizika huko Dalian, China
Watalii watembelea eneo lenye mandhari nzuri la Mlima Fairy la Chongqing, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma