Lugha Nyingine
Liu Yang ashinda medali ya kwanza ya dhahabu ya China?ya jimnastiki katika michezo ya Olimpiki ya Paris
PARIS - Liu Yang ameshindia medali ya kwanza ya dhahabu ya China ya jimnastiki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris 2024 siku ya Jumapili alipoongoza kwa hatua zote ushindi wa mchezo wa wanaume wa kujiviringisha na kunyumbua viungo kwa kutumia mikono iliyoshika pete ambapo bingwa huyo mtetezi amepata pointi 15.300 kuongoza kumaliza 1-2 kwa China katika mchezo huo.
Mwenzake wa China, Zou Jingyuan ametwaa medali ya fedha kwa kupata pointi 15.233, huku mshindi wa medali ya shaba wa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo Mwaka 2020, Eleftherios Petrounias wa Ugiriki, ambaye amepata pointi 15.100.
Samir Ait Said, mwanamichezo pekee wa kiume anayewakilisha nchi mwenyeji Ufaransa katika jimnastiki za ustadi, amemaliza wa nne kwa kupata pointi 15,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma