久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Wairan wenye kuomboleza kwa huzuni wamuaga kiongozi mkuu wa Hamas, wakiapa kulipiza kisasi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 02, 2024
Wairan wenye kuomboleza kwa huzuni wamuaga kiongozi mkuu wa Hamas, wakiapa kulipiza kisasi
Watu wakishiriki shughuli ya kusindikiza mwili wa mkuu wa ofisi ya siasa wa Kundi la Hamas aliyeuawa Ismail Haniyeh mjini Tehran, Iran, Agosti 1, 2024. (Xinhua/Shadati)

TEHRAN - Watu kutoka makundi mbalimbali ya mji mkuu wa Iran, Tehran siku ya Alhamisi walifanya shughuli ya ibada ya kumbukumbu ya Mkuu wa Ofisi ya Siasa wa Kundi la Hamas, Ismail Haniyeh aliyeuawa katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na Israel siku moja kabla ambapo shguhuli hiyo ilianza rasmi saa 2:00 asubuhi kwa saa za huko. (0430 GMT) katika Chuo Kikuu cha Tehran.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei aliongoza ibada hiyo ya kumbukumbu ya mkuu huyo wa Hamas na mlinzi wake, ambaye pia aliuawa katika shambulizi hilo hilo.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na makamanda na viongozi wakuu wengi wa Iran, akiwemo Rais Masoud Pezeshkian, Spika wa Bunge Mohammad Baqer Qalibaf na Mkuu wa Mahakama Gholamhossein Mohseni-Ejei, pamoja na idadi kubwa ya waombolezaji.

Kabla ya ibada hiyo, Qalibaf alitoa salamu za rambirambi kutokana na tukio hilo la kusikitisha na kusema, "Ni wajibu wetu kulipiza (mauaji ya Haniyeh) katika mahali na wakati unaofaa."

Israel italipa "gharama kubwa kwa shambulizi lake la woga dhidi ya eneo salama la Iran," Qalibaf amesisitiza.

Baada ya ibada hiyo, Khamenei alikutana na watoto wa Haniyeh na maafisa wa Hamas.

Kwenye shughuli ya kusindikiza mwili kwenda kwenye ibada ya kumbukumbu, idadi kubwa ya Wairan wakiwemo maafisa na makamanda wakuu wa kijeshi, waliusindikiza mwili wa kiongozi huyo wa Hamas kutoka Chuo Kikuu cha Tehran hadi kwenye uwanja wa Azadi katikati mwa Tehran, huku wakitamka kaulimbiu za kulaani Israel na Marekani, wakiwa wamebeba picha ya Haniyeh, kiongozi wa Iran na Jenerali Qassem Soleimani, kamanda mkuu wa Iran aliyeuawa katika shambulizi lililofanywa na Marekani nchini Iraq Januari 2020, na kupeperusha bendera za Iran na Palestina.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye shughuli hiyo, maafisa hao wa Iran wamesema kuwa bila shaka Israel itaadhibiwa kwa "kitendo chake hicho cha kigaidi."

Iran imeishutumu Israel kwa kutekeleza mauaji hayo huku Israel ikiwa bado haijathibitisha kuhusika kwake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>