Lugha Nyingine
China yatoa wito wa kutaka ASEAN kushikilia matarajio ya amani, njia ya ASEAN na kuhimiza amani na utulivu wa kikanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihudhuria mkutano wa 31 wa mawaziri wa mambo ya nje wa Baraza la Kikanda la Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) huko Vientiane, Laos, Julai 27, 2024. (Picha na Kaikeo Saiyasane/ Xinhua)
VIENTIANE - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi siku ya Jumamosi kwenye mkutano wa 31 wa mawaziri wa mambo ya nje wa Baraza la Kikanda la Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki, ASEAN huko Vientiane, mji mkuu wa Laos, ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa ASEAN, ametoa wito kwa nchi za ASEAN kuendelea kushikilia matarajio ya amani na njia ya ASEAN ili kudumisha amani na utulivu wa kikanda.
Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), kwenye mkutano huo amesisitiza kuwa, dunia ya hivi leo inakumbwa na misukosuko na machafuko, na migogoro ya kikanda imeendelea kwa muda mrefu, makabiliano ya siasa za kijiografia yanazidi kuwa makali, na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ugaidi na usalama wa mtandao zinatokea bila kusita.
Maamuzi ya upande mmoja na mawazo ya Vita Baridi vinaongezeka, pamoja na "miduara midogo" zaidi za kijeshi na kiusalama, amesema.
Katika kukabiliana na changamoto hizo zilizopo, waziri huyo wa mambo ya nje wa China ametoa mapendekezo kwenye mkutano huo, na kusisitiza kuwa Baraza la kikanda la ASEAN, likiwa jukwaa muhimu la mazungumzo ya pande nyingi kuhusu usalama katika eneo la Asia-Pasifiki, limetoa mchango muhimu kwa amani na utulivu wa kikanda.
Wang ametoa wito kwa nchi hizo kushikilia matarajio ya amani. Amesisitiza haja ya kufuatilia maslahi na matarajio ya pande zote na kutafuta usalama wa pamoja, wa pande zote, wa ushirikiano na endelevu.
Amesema, "mkakati wa Indo-Pasifiki" unaoongozwa na Marekani umeleta hali ngumu ya usalama, na kwenda kinyume na matarajio ya amani na ustawi wa muda mrefu katika kanda hiyo.
Wakati huo huo, Wang amehimiza kuwa na tahadhari na kupinga uingiliaji wa Jumuiya ya NATO dhidi ya kanda hiyo, amesema uingiliaji huo hakika utasababisha mapambano na kuifanya hali izidi kuwa ya wasiwasi.
Inahitajika kushikilia Njia ya ASEAN, kuongeza hali ya kuaminiana kwa kupitia mazungumzo na kuhimiza usalama kupitia ushirikiano, Wang amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma