Lugha Nyingine
China ni mshirika muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Brazil: Rais wa Brazil
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akihudhuria mkutano na waandishi wa habari wa kigeni mjini Brasilia, Brazili, Julai 22, 2024. Picha na Lucio Tavora/Xinhua)
BRASILIA - China ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Brazil, na Brazil inatarajia kujenga "ushirikiano mpya wa kimkakati" kati ya nchi hizo mbili, amesema Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva siku ya Jumatatu kwenye mkutano na waandishi wa habari wa kigeni.
Katika mkutano huo, Lula alijibu swali kutoka Shirika la Habari la China, Xinhua akisema ana nia ya kutafuta uhusiano "wa karibu sana" na China.
Ukuaji wa uchumi wa China katika miaka 40 iliyopita umetambuliwa na Brazil ina mengi ya kujifunza kutoka kwa uzoefu wa maendeleo ya China, amesema Lula akiongeza kuwa China ni mshirika muhimu kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya Brazil.
Kiongozi huyo wa Brazil amesema atashiriki kama mgeni mwalikwa kwa mara ya kwanza katika Baraza la Ushirikiano wa Kiuchumi la Asia na Pasifiki litakalofanyika Novemba Mosi mjini Lima, Peru, ambapo amepanga kujadiliana na maofisa wa China kuhusu uwezekano wa Brazil kujiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.
“Nataka kujua...tutakuwa na nafasi gani, kwa sababu hatutaki kuwa wachezaji wa kukaa benchi, tunataka kuwa kwenye kikosi cha wachezaji wanaoanza,” amesema Lula.
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akihudhuria mkutano na waandishi wa habari wa kigeni mjini Brasilia, Brazili, Julai 22, 2024. Picha na Lucio Tavora/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma